Leviticus 23:1-6

Sikukuu Zilizoamriwa

1 Bwana akamwambia Musa, 2 a“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Hizi ndizo sikukuu zangu zilizoamriwa, sikukuu zilizoamriwa za Bwana, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu.

Sabato

3 b“ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yoyote. Popote mnapoishi, ni Sabato kwa Bwana.

Pasaka Na Mikate Isiyotiwa Chachu

(Hesabu 28:16-25)

4 c“ ‘Hizi ni sikukuu za Bwana zilizoamriwa, makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilizoamriwa: 5 dPasaka ya Bwana huanza jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. 6 eSiku ya kumi na tano ya mwezi huo wa kwanza, Sikukuu ya Bwana ya Mikate Isiyotiwa Chachu huanza; kwa siku saba, mtakula mikate isiyotiwa chachu.
Copyright information for SwhKC